SUALA LA UPOTEVU WA MAJI (NRW) LIFANYIWE KAZI ZAIDI -PROF.KITILA MKUMBO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo (Mb) amesema hali ya upatikanaji wa maji imezidi kuongezeka mjini na vijijini na kwa kasi ilivyo na malengo yaliyowekwa na serikali yatafikiwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini.
.
"Takwimu za hali ya upatikanaji wa maji inatokana na uwekezaji unaofanywa na serikali katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi" alisema.
.
Prof.Kitila ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Maji 2024 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji Mhe.Prof.Kitila amesema lengo kubwa la Serikali ni kukuza uchumi shindani na kuleta maendeleo ya watu na huduma ya maji ni moja ya jambo muhimu katika kufanikisha hatua hiyo hapa nchini.
“Watendaji wa Sekta ya Maji wanafanya kazi kubwa na nzuri, tena usiku na mchana kwa ajili ya wananchi” alisema Prof.Kitila.
.
Waziri Kitila amesema kuwa Waziri wa Maji halali akipambania masuala ya maji kufika katika makazi ya wananchi.
Mhe.Prof.Kitila amesisitiza suala la upotevu wa maji (NRW) lifanyiwe kazi zaidi kwa sababu linaongeza gharama za uendeshaji na Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji wapimwe katika hatua wanazochukua kuzuia upotevu wa maji.
Aidha,Prof.Kitila ameipongeza kazi ya utunzaji na uendelezaji wa vyanzo vya maji hapa nchini hatua ambayo moja ya matunda yake ni kujaa mapema kwa maji katika bwawa la kufua nishati ya umeme la Nyerere, kabla ya muda uliokisiwa ambapo kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wa Sekta ya Maji ni moja ya hatua zilizoitoa Tanzania kimasomaso katika mradi huo mkubwa.
.
Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) Haji Nandule amekabidhi hundi ya shilingi milioni 800 kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda baada ya kuwa mamlaka ya kwanza kukidhi vigezo vya mkopo nafuu unaotolewa kwa ushirikiano na Benki ya Uwekezaji (TIB).
NWF inatoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji hapa nchini na imefungua dirisha la mikopo ya masharti nafuu kwa kushirikiana na Benki ya TIB.
@wizarayamajitz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

