logo

ASKARI 296 WA JESHI LA UHIFADHI WANYAMAPORI NA MISITU WAHITIMU MLELE MKOANI KATAVI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dastun Kitandula (Mb) amewataka Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi zote za Jeshi la Uhifadhi nchini kuhakikisha Askari wanaohitimu mafunzo watumike ipasavyo katika kuchochea kasi ya mapambano dhidi ya ujangili wa Wanyamapori na rasilimali za Misitu.

Mhe. Kitandula ametoa rai hiyo leo Machi 23, 2024 wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa Askari 296 wa jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu katika Kituo cha mafunzo cha Mlele, Mkoani Katavi.

Kitandula ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa askari yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo viovu kwa namna moja ama nyingine atachukuliwa hatua kali za kisheria

Kwa upande mwingine,Naibu Waziri Kitandula amezitaka Taasisi zinazounda Jeshi la Uhifadhi kuzingatia maelekezo yaliyotolewa awali kwa kutenga fedha kwenye bajeti zake kwa ajili ya kukarabati na kuboresha miundombinu iliyopo pamoja na kujenga miundombinu mingine mipya ili iendane na mahitaji ya kituo na mafunzo yanayotolewa.

“Ni matumaini yangu kwamba katika mwaka wa fedha ujao (2024/25) kituo hiki kitajengewa mazingira bora ya miundombinu kulingana na mahitaji ya sasa katika kuimarisha Uhifadhi wa rasilimali za Wanyamapori na Misitu hapa nchini,” alisema.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo CP.Benedict Wakulyamba amewaasa askari hao kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao,na pia amesema jukumu la askari hao ni kutoa huduma ya kulinda Rasilimali za nchi hii hivyo waitende kazi hiyo kwa uweledi mkubwa.

Aidha, Wakulyamba amesema kuwa jukumu la Jeshi la uhifadhi ni kuwa n nidhamu,uaminifu na uadilifu, huku akiwataka askari hao kuyafuata hayo ili kufanikiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn