logo

MRADI WA HEET - NM-AIST KUBORESHA MITAALA KUENDANA NA SOKO LA VIWANDA

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, chini ya Mradi wa HEET, imefanya kikao cha siku mbili wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda mnamo Machi 26–27, 2024, ili kuthibitisha mitaala yake iliyofanyiwa mapitio kuiwezesha kukidhi mahitaji ya soko.

Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi - Taaluma Utafiti na Ubunifu Prof. Anthony Mshandete kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Taasisi, amesisitiza dhamira ya taasisi hiyo katika kutoa elimu ya hali ya juu kwa wanazuoni wake katika kutatua changamoto na kutafuta majawabu kwa ajili ya viwanda.

"Maarifa kutoka kwa kamati hii katika kuunda mitaala na mwongozo wa ushiriki na changamoto za kijamii ni muhimu kusaidia taasisi kupata mitaala bora na kuzalisha wataalamu wenye uwezo madhubuti na taasisi inalenga kuhudumia jamii na kukuza maendeleo endelevu ya taifa. Kamati inatumika kama daraja kati ya wasomi, tasnia na jamii" amesema Prof. Mshandete.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi - Mipango Mipango Fedha na Utawala na Mratibu wa HEET katika Taasisi ya Nelson Mandela Prof. Suzana Augustino ameangazia malengo ya Mradi wa HEET: kuzalisha wasomi wenye ujuzi na kupitia mitaala na kuifanya ya kisasa ili kukidhi mahitaji ya viwanda.

Mkutano huo umepitia mitaala iliyofanyiwa maboresho kuhakikisha inawiana na mahitaji ya soko la kisasa kabla ya kuwasilishwa kwenge Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn