logo

MBUNGE OLE SENDEKA ALIPONGEZA SHIRIKA LA UCRT KWA KUJA NA MRADI MPYA WA KUWEZESHA VIJIJI 14 SIMANJIRO NA KITETO

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dkt.Suleiman Serera amelipongeza shirika lisilo la Kiserikali la Ujamaa Community Resource Team (UCRT) kwa kuja na mradi mpya wa kuwezesha Vijiji 14 vya Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na Kiteto kuingia kwenye Mpango wa matumizi bora ya ardhi, hali itakayosaidia kuondokana na Migogoro mingi ya ardhi Wilayani humo.

Dkt.Serera ameyasema hayo siku za hivi karibuni kwenye mapokezi ya mradi mpya wa Uhifadhi Jumuishi wa Mazingira na kuboresha maisha ya Jamii katika Halmashauri mbili za Mkoa wa Manyara ambayo ni Simanjiro na Kiteto, na kuzinduliwa katika Mji Mdogo wa Orkesument, mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Baraka Kanunga, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Christopher Ole Sendeka, Mratibu wa Shirika hilo Edward Loure, pamoja na madiwani, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji, viongozi wengine pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali.

Dkt.Serera amesema Shirika la UCRT ni shirika linalofanya vizuri sana ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro katika kuhakikisha inawafikia jamii moja kwa moja na kugusa matatizo yao na hatimaye kuweza kupanga matumizi bora ya ardhi na kuondokana na Migogoro mingi na hatimaye kuwezesha jamii za asili kumiliki, kusimamia ardhi na kunufaika nayo ili kuboresha maisha yao.

"Niwapongeze ndugu zetu wa UCRT chini ya Mratibu wake Edward Loure kwa kazi kubwa na nzuri, ambayo mnaifanya na mnaendelea nayo kuzifanya,katika Wilaya yetu ya Simanjiro na Kiteto, kwasababu tunaona matokeo yake mazuri na makubwa yamechangia hata kuondoa baadhi ya Migogoro mkubwa ya ardhi tuliyokuwa nayo katika Wilaya hizi " alisema Dkt.Serera.

Aidha,Dkt.Serera amesema hakuna jambo gumu Duniani kama kumshawishi mzungu kwa lugha yake akupatie pesa yaani hilo ni jambo gumu sana lakini Mratibu wa UCRT Edward Loure ni jambo kubwa sana linalohitaji pongezi kubwa, hivyo Viongozi mbalimbali kwenye maeneo husika wahakikishe wanatoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha suala hilo kikamilifu na si vinginevyo.

.

Dkt.Serera anasema miaka ya nyuma ukiitaja Wilaya ya Kiteto, Simanjiro kwa mambo ya Migogoro ya ardhi na hata watu kuzuriana ilikua kazi kubwa sana , lakini UCRT imefanya kazi kubwa na bidii waliyoionyesha kwa kupima kupata matumizi bora ya ardhi wamefanya namna njia inavyoenda na hatimaye wamepunguza kwa kiasi kikubwa sana Migogoro ya ardhi.

.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Christopher Ole Sendeka amempongeza Mratibu wa mradi huo Edward Loure kwa mambo makubwa ya msingi ya maana sana, awali zaidi ya Vijiji 30 vimeingia katika matumizi bora ya ardhi na sasa Vijiji 9 pia vimo, hilo ni jambo kubwa sana kwa Maendeleo endelevu ya Wana Simanjiro.

"Mradi huu unakwenda kutoa elimu kwa wananchi, unatoka elimu ya Sera, sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia masuala ya ardhi na wakati mwingine biblia inasema ukishaijua kweli na hiyo kweli itakuweka kuwa huru, nina maana wakati mwingine wananchi wetu wakishajua sera ya nchi inasema Nini katika masuala ya ardhi , Mazito, mifugo basi watakua wapole tu maana tayari wameshaelimishwa na shirika la UCRT, hivyo hongera sana mdogo wangu Edward Loure" Alisema.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn