MIAKA 60 YA MUUNGANO, TUMEFANIKIWA KUZIPANDISHA KWENYE LIGI KUU TANZANIA BARA TIMU ZA MAJESHI - WAZIRI DKT.STERGOMENA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe.Dkt.Stergomena Tax amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano,Wizara ya Ulinzi imefanya vizuri sana kwenye upande wa michezo ambapo timu za Majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT zimefanikiwa,ikiwemo Timu ya Mashujaa FC iliyopo Kigoma iliyofanikiwa kupanda ligi Kuu Tanzania
Bara na kuungana na timu ya JKT Tanzania.
.
Dkt.Stergomena ameyasema hayo leo April 03,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Kuhusu Mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
.
Amesema Wizara hiyo pia
imefanya vizuri katika Mashindano ya kimataifa ya Riadha ya ndani na nje ya
nchi na kushinda nafasi mbalimbali katika mashindano hayo.
.
"Mwaka 2023, timu ya riadha, ilishiriki mashindano ya Majeshi ya Dunia
nchini Uswisi ambapo Sajini Alphonce Simbu alishika nafasi ya Pili,na
Sajinitaji Ezekiel Jafari Ng’imba alishika nafasi ya pili katika mbio za km 42
za Sahel Military Marathon, Abuja (Nigeria) mwaka 2021" alisema Dkt.Stergomena.
.
Waziri Stergomena amesema kupitia Wizara hiyo,wameendelea kuboresha maslahi kwa wanajeshi na watumishi wa Umma kadri uwezo wa kifedha unavyoruhusu ambapo mpaka hivi sasa Serikali imekwisha jenga nyumba za makazi katika kambi mbalimbali za Jeshi kwenye Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,Dodoma,Kagera, Kigoma, Morogoro, Mwanza,Pemba,Pwani, Rukwa, Tabora,na Tanga.
.
Amesema eneo jingine ambalo wizara ya Ulinzi imefanikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za afya na tiba kupitia hospitali za Jeshi za Kanda ambazo ni Lugalo Dar es Salaam, MH Mwanza, Bububu Zanzibar, Mirambo Tabora, MH Arusha, MH Mbeya ambazo hutoa
huduma kwa wanajeshi, na pia kwa wananchi waishio maeneo yaliyo jirani na kambi za Jeshi,na takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wanaopata huduma katika hospitali za Jeshi ni raia.
.
Aidha, Waziri Stergomena amesema Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ni jambo muhimu kwa Taifa, hivyo Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele katika ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, na Ujenzi huo unatekelezwa na wataalam wa ndani ya nchi,kwa gharama ya Serikali.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

