WADAU TOENI USHIRIKIANO KATIKA KUBORESHA MPANGO WA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU -PROF.CALORYNE NOMBO
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Caloryne Nombo amewataka Wadau wa sekta ya Elimu kujadili kwa kina Mawasilisho na kutoa maoni yenye tija katika kuboresha Elimu nchini na kuchagiza Mageuzi katika sekta hiyo.
.
Prof.Nombo ameyasema hayo April 03,2024 Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Mkutano wa mwaka wa pamoja wa Tathmini ya Sekta ya Elimu 2022/2023,unaolenga kupitia na kuchambua Utekelezaji wa vipaumbele vya mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu.
Katibu Mkuu huyo amewaeleza Wadau hao kuwa Wizara imefanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Elimu na kuanza utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Amesema kuwa maboresho ya Mitaala katika ngazi ya Elimu ya kati na Elimu ya Juu yanaendelea na kwamba Wadau mbalimbali watafikiwa ili kutoa maoni.
.
Aidha, Prof.Nombo amesema Wizara hiyo imechukua hatua za makusudi za kusasisha mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu 2021-2022 hadi 2025-2026 ili kuendana na mabadiliko ya Sera na Mitaala, pamoja na Takwimu mbalimbali kwa kuzingatia Matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022.
.
"Kazi hii inafanywa na wataalamu wabobezi kutoka ndani na nje ya nchi yetu na kwa kushirikisha wadau wa elimu ambao wapo ndani ya nchi na Nje ya nchi yetu" alisema Prof.Nombo.
.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dkt.Daniel Baheta ameahidi Serikali kuendeleza ushirikiano kuhakikisha Watoto wa kitanzania wanapata Elimu bora.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Tanzania Education Network (TENMET) Faraja Nyalandu amesema Mkutano huo utawasaidia kuja na mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya Elimu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

