logo

MADARAJA MAKUBWA 8 YAMEKAMILIKA MIAKA 3 YA RAIS SAMIA MADARAKANI -WAZIRI BASHUNGWA

Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa amesema katika kipindi cha miaka mitatu tangu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aingie madarakani,Sekta ya Ujenzi imefanikisha ujenzi wa madaraja makubwa 8 yakiwemo Daraja la Wami mkoani Pwani, Daraja la Tanzanite mkoani Dar es Salaam, Daraja la Gerezani mkoani Dar es Salam, Daraja la Mpwapwa mkoani Dodoma, Daraja la Kiegeya mkoani Morogoro, Daraja la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Daraja la Kitengule mkoani Kagera na Daraja la Msingi mkoani Singida.

.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo April 05,2024 jijini Dodoma kwenye hafla ya kuelezea mafanikio ya Sekta ya Ujenzi katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan madarakani.

Vilevile, Bashungwa ameeleza kuwa madaraja matano yapo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji ikiwemo Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) mkoani Mwanza ambao umefikia 85%, Daraja la Pangani mkoani Tanga umefikia 23%, Daraja la Mbambe mkoani Pwani umefikia 15% na Daraja la Mpiji Chini mkoani Dar es Salaam.

Kuhusu utekelezaji wa Viwanja vya Ndege, Waziri Bashungwa amesema kuwa Sekta ya Ujenzi imekamilisha Viwanja vya Ndege 5 vikiwemo Kiwanja Cha Ndege cha Geita, Mwanza, Mtwara, Songwe na Songea.

.

Amesema mpaka hivi Sasa Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami wenye jumla ya kilometa 1,198.50 katika kipindi cha miaka mitatu cha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani mwezi Machi, 2021.

.

“Katika kipindi cha miaka hii mitatu, barabara 25 zimekamilika na 57 zenye urefu wa kilometa 3,794.11 zinaendelea na zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji”, alisema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Wizara ya Ujenzi imetenga miradi itakayotekelezwa na wazawa kwa lengo la kuwajengea uwezo makandarasi na Wahandisi Washauri elekezi wa ndani.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn