Top news
PPRA YATOA TUZO ZA MIKATABA ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.95 KWA MAKUNDI MAALUM
Mkurugenzi Wa Huduma za Ushauri Na Kujenga Uwezo kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi Amini Mcharo amesema hadi kufikia mwezi Februari 2024, jumla ya tuzo za mikataba zenye thamani ya shilingi bilioni 1.95 zimetolewa kwa makundi maalum kupitia zabuni za umma zilizotangazwa na taasisi nunuzi kupitia mfumo wa NeST ambapo kundi la vijana wamepata tuzo za mikataba zenye thamani ya shilingi milioni 709, wanawake shilingi bilioni 1.2 na wazee shilingi milioni 78.3.
.
Mhandisi Mcharo ameyasema hayo leo April 09,2024 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari juu ya Mafanikio ya Miaka 3 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mageuzi Makubwa katika Ununuzi wa Umma Nchini.
.
Amesema Zaidi ya shilingi trilioni 29 zimewekwa kwenye mfumo wa NeST kwa ajili ya kufanya ununuzi wa bidhaa, huduma na kazi za ujenzi.
"Hadi kufikia Aprili 09,2024, mikataba ya zaidi ya shilingi trilioni 5.14 imetolewa kwa wazabuni kupitia mfumo wa NeST, ambapo wazabuni 18,101 wamejisajili kwenye mfumo huo" alisema Mhandisi Mcharo.
.
Mhandisi huyo amesema Mamlaka hiyo imekamilisha tafiti ndogondogo katika matumizi ya taratibu ya ununuzi kwa njia ya Force Account ambapo ilibainika kuwa kuna matumizi ya njia hii yasiyoendana na sheria na kanuni inavyoelekeza na sheria mpya ya ununuzi ya mwaka 2023 imeboresha matumizi ya utaratibu huo.
Mcharo amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, Mamlaka ilifanya uchunguzi kwa zabuni zilizotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, na kufanikiwa kuokoa jumla ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 16.27.
Aidha, Mhandisi huyo amesema Sheria ya Ununuzi wa Umma, imeweka masharti muhimu yatakayohakikisha uwepo wa upendeleo wa bidhaa na wazabuni wa ndani, ambapo inatarajiwa kuwa zabuni zote zilizo chini ya shilingi bilioni 50 zitafanywa na wazawa.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

