logo

MBUNGE FATMA TOUFIQ ATOA SADAKA YA FUTARI KWA WATOTO YATIMA JIJINI DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe.Fatma Toufiq ametoa sadaka ya futari kwa vituo vya kulelea Watoto Yatima vilivyopo jijini Dodoma ili kuwawezesha kutimiza nguzo muhimu ya uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Msaada ambao ameutoa ni Sukari,Ngano,Mafuta ya kula ambapo vyakula hivyo vitawasaidia katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mbunge huyo amewahimiza watoto hao kuzingatia maadili na masuala ya dini na waendelee kulingania Uislamu.

"Msome kwa bidii ili kusudi muweze kufanikwa muwezekuwa na shughuli zenu lakini pia mzingatie masuala ya dini na maadili na muendelee kuulingania uislamu nawatakieni kila la kheri" alisema Mbunge Fatma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn