logo

MBARAWA: HAKUNA MIRADI YA UJENZI KUSIMAMA

SERIKALI imetoa Maagizo Kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege kuhakikisha wanaendelea na utekelezaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa viwango na kwa muda uliopangwa.

Agizo hilo limetolewa mkoani Rukwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya NtendoMuzeKilyamatundu (km 179) awamu ya kwanza inayoanzia Ntendo - Kizungu (km 25) kwa kiwango cha lami.

Mbarawa Amesema kuwa kuhusu suala la malipo Serikali inatambua na itaendelea kuhakikisha inakamalisha taratibu za malipo mara tu baada ya wakandarasi kuwasilisha hati za madai.

"Serikali inapokea madai ya wakandarasi na kuna taratibu za uhakiki ilizojiwekea ili kujiridhisha hivyo TANROADS endeleni kuwasimamia wakandarasi wote nchini tuikamilishe miradi", Alisema Mbarawa.

Aidha, Waziri Huyo Amesema hivi karibuni Serikali itaweka historia kwa kusaini mikataba ya EPC + F ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 2,000 kwa ajili ya kuunganisha mikoa yote kwa kiwango cha lami.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila, Amesema mkataba wa ujenzi wa mradi huo umetolewa kwa kampuni ya China Geo - Cooperation ya nchini China ambapo mkataba ulisainiwa tarehe 29 Machi 2022 na mradi ulianza tarehe 6 Juni 2022 kwa muda wa miezi 18 pamoja na miezi 12 ya matazamio.

Kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Rukwa Eng.Mgeni Mwanga, amesema mradi huo utajumuisha ujenzi wa makalvati makubwa 17 na makalvati madogo 43 ambapo hadi sasa makalvati makubwa 4 yamekamilika na 9 ujenzi unaendelea huku makalvati madogo 5 yamekamilika na yaliyobakia yanaendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendinga amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwani inapita kwenye maeneo yenye fursa mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji wa madini (makaa ya mawe) na uchimbaji wa gesi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn