logo

NELSON MANDELA NA SIMON FRASER WAENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA KUBADILISHANA UTAALAM

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof.Maulilio Kipanyula amekutana na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Simon Fraser cha nchini Canada na Chuo Kikuu cha Aga Khan leo Mei 02,2024 Jijini Arusha.

Prof.Kipanyula amesema lengo la kukutana ni kuendelea kuimarisha ushirikiano katika programu za kubadilishana wasomi na wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya makubaliano.

Kwa upande wake Prof.Woo Soo Kim kutoka Chuo Kikuu cha Simon Fraser amesisitiza umuhimu wa kupokea maoni kutoka kwa wadau na watumiaji wa mwisho wa bunifu na teknolojia zinazoibuliwa na wanafunzi na wabunifu mbalimbali.

Aidha,ziara hiyo na warsha ya siku moja ambapo wanafunzi wa SFU na NM-AIST waliwasilisha mada na tafiti katika masuala ya Maendeleo ya teknolojia katika kilimo na mazingira.

Katika hatua nyingine Wanafunzi na viongozi kutoka Chuo Kikuu cha Saimon Fraser pia walipata fursa ya kutembelea maeneo muhimu ya Taasisi ikiwemo kuonyeshwa madhari mazuri yanayozingatia utunza wa mazingira, Maabara,Hosteli, kituo Atamizi na Maktaba.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn