Top news
SAMIA: KILA MWAKA TUTAKUWA NA NYONGEZA ZA MISHAHARA
RAIS Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Amesema Wafanyakazi Wote Mwaka Huu mbali Na Yale Aliyoyasema Kuhusu Posho, Mishahara Nk.Kutakuwa Na Nyongeza Za Mishahara za Kila Mwaka na Tayari wameanza Mwaka Huu na Itafanyika Kila Mwaka kama Ilivyokuwa Zamani.
.
Samia Ameyasema Hayo Leo Mei 01,2023 Katika Kilele Cha Maadhimisho Ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa 2023 yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
.
Amesema Mwaka Huu 2023 Kutakuwa Na Mavuno Makubwa Ya Upandishaji Wa Viwango Vya Posho Na Kuhusu Mishahara Amesema Mbali Na Posho alizozisema kama Serikali wamejipanga Kuendelea Kupandisha Madaraja, Vyeo Nk.
.
"Yale Madaraja Ya Mserereko Ambao hawakupata Mwaka Uliopita Mwaka Huu pia Kutakuwa Na Mserereko, Lakini Niseme Pia Kuna Nyongeza Za Mwaka ambazo Kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa nikaona Mwaka Huu nizirudishe" Amesema Samia.
.
Kuhusu Masuala Ya Makato Ya Kodi, Na Marupurupu Samia Amesema Amemuachia Waziri Wa Kazi, Waziri Wa Fedha Na Vyama Vya Wafanyakazi wakae Chini waangalie kama Kuna Yale ambayo Sio Vyema Kuyakata Kodi Waache Kukata Kodi.
.
Aidha, Samia Amesema Suala la Waajiri Kutokuwasilisha Michango Ya Wafanyakazi Kwa Wakati ameongea Na Waziri Mkuu ambapo Amesema ataitisha Mkutano na Waajiri Ili Kulizungumzia Suala Hilo na Waajiri wawasilishe Michango Kwa Wakati Hasa wale Ambao wamepewa Fedha Na Serikali halafu hawawasilishi.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

