logo

ZAIDI YA ASILIMIA 95 YA WAKAZI WA MIJINI WATAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA IFIKAPO MWAKA 2025 -WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini umefikia wastani wa asilimia 90 mwezi Desemba 2023 kutoka wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022.

.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Mei 10,2024 alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Amesema Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa miradi ya maji 85 inayohudumia wakazi 4,641,505 wa maeneo ya mijini huku Dhamira ya Serikali ni kuona, zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.

"Kwa mwenendo huu, kwa uongozi mahiri wa Mama Samia na kwa ushirikiano mkubwa wa Bunge lako na ufuatiliaji wa Waheshimiwa Wabunge, Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 iliyotuelekeza kufikia zaidi ya asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini inatekelezwa barabara.

"Narudia, Ilani ya Chama Tawala inatekelezeka barabara. CCM ndiyo mwenye duka, sisi wauza duka, tutatimiza wajibu wetu mchana na usiku, iwe mvua, liwe jua na kwenye mabonde na milima" alisema Aweso.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn