TAWA YAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU UKEREWE
Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Serema kata ya Bwiro wilayani Ukerewe wanaoishi pembezoni mwa ziwa Victoria lengo ikiwa ni kuwasaidia kujikinga na majanga ya uvamizi wa wanyama aina ya mamba na viboko ambao wamekuwa wakiathiri maisha ya wananchi ambao baadhi yao hupoteza uhai.
Hayo yamejiri kufuatia wakazi wa maeneo mbalimbali hapa nchini kutochukua tahadhari za mara kwa mara katika kujilinda na wanyama wakali ambao ni hatarishi kwa maisha yao.
Afisa Habari wa mamlaka ya Usimamizi wanyama Pori Tanzania (TAWA) Beatus Maganja ambaye amewaeleza wananchi hao kuwa serikali imejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wanakuwa salama.
"Katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu Serikali inahakikisha usalama wa mwananchi unakuwa ni kipaumbele cha kwanza na ndiyo maana mara kwa mara Maofisa wa TAWA wamekuwepo maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu na kufanya doria katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa na changamoto ya wanyamapori hao" alisema Maganja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Joshua Manumbu ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) kwa elimu wanayoendelea kuitoa katika jamii namna ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko na kuwadhibiti pale wanapoonekana kuhatarisha maisha ya wananchi.
.
Kwa upande wao,wananchi wa Kijiji cha Selema kilochopo Kata ya Bwiro wilayani humo wameipongeza na kuishukuru TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa wilayani humo ambayo wamekiri kuwa imekuwa msaada kwao na itawawezesha kuendelea na shughuli zao za kiuchumi huku wakiepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori hao.
Mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania TAWA imekuwa ikitoa elmu maeneo mbalimbali hapa nchini lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi wanaoishi maeneo hatarishi dhidi ya wanyama hao.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

