logo

WATOTO WA KIUME ASILIMIA 45% WAMEATHIRIKA NA UKATILI WA KINGONO MWAKA 2023 - DKT.ANNA HENGA

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt.Anna Henga amesema katika ripoti yao waliyoizindua mwezi April mwaka huu, mwenendo wa Haki za Binadamu hapa nchini umedorola kwa mwaka 2023 ukilinganisha na mwaka 2022,huku akiyataja makundi yaliyoathirika zaidi kuwa ni kundi la watoto asilimia ambalo limeathiriwa kwa asilimia 45%, wanawake asilimia 30%,watu wenye ulemavu asilimia 10%, wazee asilimia 12% na wanaume asilimia 10%.

.

Dkt.Anna ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano ulioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu uliofanyika Mei 11, 2024 Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili kwa pamoja masuala yanayogusa haki za binadamu.

.

"Kwahiyo imedorola kwa kiasi hicho na kundi linaloathirika zaidi ni la watoto huwa tunalisahau sana, Watoto wetu wanafanyiwa ukatili mkubwa wa kingono,ubakaji, ulawiti na Katika watoto pia, watoto wa kiume ndio wameathirika zaidi Asilimia 80 na ulawiti. Na asilimia 85 wanalawitiwa wakiwa nyumbani na ndugu wa karibu na Sisi kama Watu Wa Haki za Binadamu lazima tutalifanyia Kazi Suala hilo" alisema Dkt.Anna.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn