WABUNGE HAMASISHENI HALMASHAURI ZITUMIE MFUMO WA NEST - BW.ELIAKIM MASWI
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mussa Azzan Zungu(@zungumussa) amesema Mfumo Mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST) ni mzuri na unafaa katika maslahi mapana katika taifa letu, hivyo watu wanapaswa kuwa na subira, uelewa namna gani ya kutumia Mfumo huo pale inapotokea changamoto mbalimbali ikiwemo suala la mtandao kusumbua.
.
"Muda mwingine kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa mtandao hivyo watu wasilalamike sana Mfumo kusumbua kwenye eneo hili la Mtandao, watu wanapaswa kuwa na subira" alisema.
.
Mhe.Zungu ameyasema hayo alipokuwa akifungua Semina ya Matumizi ya Mfumo Mpya wa Ununuzi wa Umma (NeST) kwa Wabunge iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) jana Juni 08,2024 Bungeni Jijini Dodoma.
.
Aidha, Zungu ameipongeza PPRA kwa kuanzisha mfumo huo kwani unasaidia kutatua changamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo kuomba fursa za tenda za Serikali nk.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Bw.Eliakim Maswi amesema mara baada ya Mamlaka hiyo kuhakikisha makundi maalum nayo yanapewa nafasi katika mfumo huo, PPRA itaziwezesha taasisi nunuzi zitangaze zabuni na kuzielekeza katika makundi maalum na hakuna mzabuni mwingine atakayeweza kuomba kazi hiyo isipokuwa makundi maalum pekee.
.
"Kwenye mfumo tumeweka System ya kulazimisha watu watangaze zabuni na mtu asiyekuwa wa makundi Maalum hawezi kuomba" alisema Maswi.
.
Aidha,Bw.Maswi amezitaka halmashauri zilizopo hapa nchini kutumia mfumo huo katika kuomba tenda kwani mpaka hivi sasa idadi ya taasisi zinazotumia NeST imekuwa ni ndogo sana jambo ambalo linasikitisha sana.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

