TUCHANGAMKIE FURSA ZA UFADHILI WA KIMASOMO ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI-DKT.KAZUNGU
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt.Khatibu Kazungu amewataka Wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Feza kuhakikisha wanatumia fursa za Ufadhili wa Masomo zinazotolewa na Serikali ili kuweza kujipatia maarifa mbalimbali na kuwezesha kuwa na Wataalamu wenye ubobevu katika sekta mtambuka.
Dkt.Kazungu ameyasema hayo Juni 15, 2024 Tegeta jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Jumanne kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari ya Feza na kuhudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali.
"Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Elimu imeendelea kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa Elimu. Zipo nafasi za Ufadhili wa Masomo katika Nchi tofauti tofauti na pia kumekuwa na ongezeka la Bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Lengo ni kuhakikisha kila Mwanafunzi anapata Elimu bora.Tutumie nafasi tuliyonayo kuchangamkia fursa hiyo" alisema Khazungu.
Vilevile, Kazungu amewahasa Wanafunzi hao kuhakikisha wanaendelea kuimarisha upendo na mshikamano na kujiepusha kujiingiza katika vitendo vinavyoweza kuwasababishaia kutotimiza ndoto zao na kutokuwa na tija katika maendeleo ya Taifa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

