PROF.NAJAT AAHIDI USHIRIKIANO ZAIDI NA WAFANYAKAZI TAEC
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof.Najat Kassim Mohammed amesema atahakikisha anashirikiana na wafanyakazi wa TAEC ili kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo kisheria na kuleta tija kwa taifa sambamba na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
.
Prof.Najat ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) jijini Dodoma baada ya kufanya kikao na wafanyakazi wote wa TAEC ikiwa ni siku chache tangu alipoteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia na Huduma za Ufundi Dkt.Remigius Kawala amesema wataungana na Prof.Najat ili kuhakikisha teknolojia ya nyuklia inaendelezwa hapa nchini.
.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TAEC, Mkuu wa kanda ya kati ya TAEC, Bw.Machibya Matulanya amesema wafanyakazi wote wapo tayari kumsaidia Mkurugenzi Mkuu kutimiza majukumu yake sambamba na kuhakikisha lengo la uwepo wa taasisi linatimia.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

