VYUO VIKUU VYAKUTANA KUJADILI UTEKEKEZAJI MTAALA MPYA WA ELIMU
Kamati ya Wakuu wa Vyuo Vikuu Tanzania (CVCPT) imekutana kujadiliana namna ya kutekeleza Mtaala Mpya ili kuendana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 kwa ngazi ya Elimu ya Juu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Juni 24, 2024 Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, mabadiliko ya sera elimu na mafunzo yataleta matokeo mazuri katika ubora wa elimu katika ngazi mbalimbali kwa kuwa imejikita zaidi katika elimu ya amali.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa ameeleza kuwa, tume hiyo ina matarajio makubwa na kamati hiyo ya Makamu wakuu wa vyuo kwa kuwa wao ni wenyeviti wa seneti za vyuo ambao ndo huwa wanaidhinisha mitaala katika elimu ya juu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msofe ameeleza kutokuwa na wasiwasi na utekelezaji wa sera na mitaala mipya kwa kuwa kamati hiyo ipo na itaifanyia kazi kwa upande wa elimu ya juu.
Kikao cha Kamati ya Wakuu wa Vyuo Vikuu Tanzania hukutana mara mbili kwa mwaka lengo ikiwa kujadili masuala ya kielimu ili kuishauri Serikali kuhusu mwenendo wa elimu ya juu nchini kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

