logo

DAWASA FUATILIENI CHANGAMOTO ZA WANANCHI KWENYE MAUNGANISHO YA MAJI -WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) makao Makuu kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kushuka ngazi za chini na kufuatilia changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo uunganishaji maji, pamoja na kuhakikisha wanawaunganishia maji Wananchi wote ambao tayari wameshalipia huduma hiyo Kwa muda mrefu.

Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo Leo Julai 2, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wananchi Kata ya Goba Wilayani Ubungo, katika mkutano uliofanyika Mtaa wa Kibululu muda mfupi baada ya kumpigia simu Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA Makao Makuu Bi. Hellen Lubogo ambaye alitakiwa kuwepo kwenye ziara hiyo, baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu changamoto hiyo ya Wananchi kulipia huduma bila kufungiwa mabomba yao.

Amesema kuwa tangu kuanza Kwa ziara yake kumekuwepo na malalamiko mengi ya Wananchi kuhusu changamoto hiyo, ambapo takribani watu 30,000 (Elfu Thelathini) wameomba kuunganishiwa maji lakini hawajaunganishwa, huku akiwasisitizia watendaji wa Mamlaka hiyo kufanya kazi Kwa moyo wa kuwasaidia Wananchi kila mmoja Kwa nafasi yake.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn