logo

PROF. NAJAT AHITIMISHA ZIARA YAKE KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof.Najat Kassim Mohammed amehitimisha ziara yake ya kutembelea ofisi za kanda ya ziwa kuzungumza na wadau wanaoshirikiana na TAEC Pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TAEC ili kujua mafanikio na changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao.

.

Prof.Najat ametembelea vituo sita ambavyo ni Kituo cha TARI – Ukiliguru, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Uwanja wa ndege jijini Mwanza, Bandari ya Mwanza, Ofisi ya Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa iliyopo Nyegezi jijini Mwanza pamoja na Ofisi ya TAEC mpakani Sirari mkoani Mara.

.

Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Sirari mkoani Mara Prof. Najat amesema ziara yake imelenga kukutana na taasisi ambazo zina ushirikiano na TAEC ili kujitambulisha pamoja na kuona maeneo ya kuongeza ushirikiano ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC).

.

Aidha,Prof. Najat ametumia nafasi hiyo kuzungumza na wafanyakazi wa kanda ya ziwa ambapo amefahamu utendaji wao wa kazi sambamba na kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili ili kuleta ufanisi eneo la kazi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn