logo

WANANCHI WA BUTIAMA WAMENITUMA KUFANYA KAZI -SAGINI

Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa kazi kubwa aliyopewa na Wananchi wa Butiama ni kulihakikishia jimbo hilo maendeleo ya kiwango cha juu katika kila eneo na sio kutumia muda wake kujibishana na Wananchi wanaotoa kauli zisizofaa na lugha chafu kwa kukosa ajenda za maendeleo za kulizungumzia Jimbo hilo.

Mhe. Sagini ameyasema hayo Julai 19, 2024 wakati akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama, kilichofanyika katika Kata ya Kukirango kijiji cha Kiabakari Butiama.

"Tumeweza kupambana Leo jengo la Halmashauri lipo na linatumika na ukamilishaji wa jengo utaendelea katika maeneo yaliyobakia. Hospitali ya Wilaya awali ilikua ni Kituo cha Afya na nilikuja na wazo la kujenga Kituo Afya. Diwani wa Butuguri, Mwenyekiti na Katibu walitafuta eneo wakatoa ekari 40 na sasa Kituo kipo kimekamilika na kinafanya kazi. Kuhusu huduma ya maji, mradi wa maji Mgango, Kiabakari, Butiama, miundombinu imekamilika ila kwa sasa mradi yapo maboresho yanayoendelea kufanywa katika maeneo ambapo mabomba yanavujisha maji na tarehe 22 mwezi huu wa Julai tunategemea ugeni wa Naibu Waziri wa Maji kwa ajili ya kuukagua huo mradi" Alisema Sagini

Aliendelea kusema, "Kuhusu Chuo cha Mwalimu Nyerere ujenzi unaendelea kwa kasi na niendelee kuwaomba Wananchi wa Butiama kuanza kufanya maandalizi ya kuchangamkia fursa katika Chuo hicho kwani kitakwenda kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Wananchi wa Butiama. Maendeleo mengi yamefanyika ujenzi wa barabara, taa za barabarani, maendeleo mengi yamefanyika Butiama na nyote ni mashahidi kazi zinaongea"Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Butiama Christopher Marwa Siagi amesema kuwa sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio wakati wa kutangaza nia au kufanya Kampeni hivyo wale wote wenye nia na nafasi hizo wasuburi muda muafaka utakapotangazwa.

Aidha, amesisitiza kuwaacha Viongozi waliopo madarakani wafanye kazi kwani mwisho wa siku kazi ndizo zitakazozungumza na si vinginevyo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn