KIJANA ENOCK AKAMATWA AKITOROKA NA SAKRAMENTI KANISANI IFAKARA
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19,Enock George Masala amekamatwa akitoroka na Sakramenti takatifu katika kanisa katoliki la mjini Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Enock, amekamatwa na walinzi wa Kanisa Kuu la Mtakataifu Andrea siku ya Jumapili ya leo Julai 28,2024 asubuhi mara baada ya kudaiwa kutekeleza uhalifu huo wa kushangaza.
Inaripotiwa kuwa,mshukiwa alipatikana akitoroka na sakramenti takatifu baada ya kupokea Ekaristi katika kanisa hilo.
Wakati ibada ikiendelea, ilitangazwa Kanisani kuhusu tukio la wizi wa Sakramenti ambayo mshukiwa alitaka kutoroka nayo.
Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo la Ifakara Padre Marcus Mirwatu, amesema kumekuwa na wimbi la matukio ya watu wasio wakatoliki wanaoingia Kanisani kukomunika na kisha kuondoka na Sakramenti, kinyume na taratibu na miongozo ya kanisa Hilo.
.
Aidha, Padre Mirwatu amelaani vitendo hivyo na kuwataka wakisto kuwafichua watu wenye tabia kama hiyo, ambao wanakwenda kinyume na imani ya kanisa hilo.
Aidha, amewataka walinzi wa kanisa kuendelea kumuhoji kijana huyo ili kufahamu sababu za yeye kufanya kitendo hicho.
"Tunashindwa kuelewa watu hawa wanatumwa na nani kufanya vitendo hivi, hatuelewi wana malengo gani kwa kanisa letu, Hivyo ninaomba kijana huyu aendelee kuhojiwa kwanini amefanya tukio Hilo" alisema Padre Mirwatu.
Kijana huyo alipohojiwa na mwandishi wa habari, alikiri kuwa yeye sio mkristo mkatoliki, na alifanya kitendo hicho baada ya kuona wakristo wengine wamepanga foleni na kupokea Sakramenti.
Aidha, Alidai kuwa hakujua kama ni kosa kuondoka na Sakramenti kanisani hapo huku akiweka wazi kuwa hakuna taratibu zote za kikanisa anazozijua.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

