logo

WAZAZI NA WALEZI SHIRIKIANENI NA WALIMU KATIKA ULINZI WA MTOTO -MTATURU

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amewahimiza wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto ili kuwaepusha na vitendo vya kikatili vinavyoripotiwa kutokea katika jamii.

Mtaturu ametoa rai hiyo Julai 29,2024, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kikio Kijiji cha Munane akiwa kwenye ziara yake ya kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti 2024/2025,kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji 2024 na kusikiliza kero za wananchi.

"Wazazi wenzangu kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha mtoto anakuwa salama,jukumu hili kila mmoja anapaswa kulitimiza,tuwalinde watoto wetu,na ili kulifanikisha hili ni lazima kuwe na ushirikiano baina ya wazazi,walezi na walimu,ujue mtoto amefika shule saa ngapi na ametoka saa ngapi,

"Pia tuwahimize watoto wetu watembee makundi makundi ili jambo lolote likitokea basi kuwe na shahidi walau wakueleza kilichotokea na hivyo kurahisisha upatikanaji wake,".amesisitiza Mtaturu.

Ziara ya Mtaturu jimboni humo inamfikisha katika kila Kijiji akibeba jumbe tatu ambapo ziara hiyo ameipa jina ya Kishindo Jimboni Kijiji kwa Kijiji.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn