JKT INATOA ELIMU BURE KWENYE KILIMO,MIFUGO NA UVUVI -MEJA JENERALI MABELE
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema JKT inawafundisha vijana wanaopitia Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na wale wa Kujitolea stadi za kazi na stadi za maisha ikiwemo namna bora ya kufanya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa tija kwa kutumia eneo dogo.
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Jambo Tanzania Kinachorushwa na Televisheni ya TBC 1 leo Agosti 08,2024 ikiwa ni Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Kwa upande mwingine, Meja Jenerali Mabele amesema kuwa, JKT imekuwa ikiendelea kutoa elimu bure ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa wananchi katika kanda zote za maonesho kwa mwaka mzima, hivyo wananchi watembelee viwanja vya Themi jijini Arusha, viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, viwanja vya Mwl JK Nyerere Mkoa wa Morogoro, viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu, viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, na wale wa mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na maeneo mengine watembelee viwanja vya Nanenane Nzuguni hapa Dodoma.
Amesema wananchi wanaopita katika Banda la JKT katika maeneo yote hayo watapata elimu, uzoefu na ujuzi wa mambo mbalimbali pamoja na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Vijana wa JKT katika Vikosi, Shule, Vyuo na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMAJKT).
.
Aidha,Meja Jenerali Mabele amewataka wananchi kutembelea maonesho ya Wakulima Nanenane katika Kanda zote za Maonesho nchi nzima kwani JKT linashiriki Maonesho hayo Kitaifa na Kikanda.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

