WATUMISHI TAEC WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU ILI KULETA TIJA KWA TAASISI
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed amewataka watumishi wa TAEC kanda ya Kaskazini kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuleta tija kwa taasisi sambamba na kuwahudumia wananchi kwa wakati.
.
Prof. Najat ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa TAEC Kanda ya Kaskazini jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kuzungumza na wafanyakazi wa kanda hiyo tangu ateuliwe na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza taasisi hiyo.
.
Prof. Najat amesema atashirikiana na wafanyakazi kupambania maslahi ya wafanyakazi wa TAEC na kuwataka kushirikiana katika kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili kusogeza gurudumu la maendeleo mbele.
.
Baadhi ya wafanyakazi wa TAEC Kanda ya Kaskazini wamempongeza Prof. Najat kwa kuteuliwa kuiongoza taasisi hiyo na kumuahidi ushirikiano katika kuhakikisha malengo ya uanzishaji wa taasisi hiyo kisheria yanatimizwa.
.
Aidha,Prof. Najat yupo katika ziara maalum ya kutembelea ofisi za TAEC Kanda ya Kaskazini ambapo tayari ametembelea ofisi ya TAEC Holili, Tarakea, Namanga na leo Ofisi za TAEC Kanda ya Kaskazini eneo la Njiro Jijini Arusha ambapo kote anapata nafasi ya kuwasililiza wafanyakazi ili kutatua changamoto zao na kuhimiza uwajibikaji kwa maslahi ya taifa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

