logo

WAZIRI AWESO AIELEKEZA DUWASA KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI ZAIDI DODOMA

SERIKALI imeiagiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) kuendelea kutafuta vyanzo mbadala vya maji hususani uchimbaji wa visima ili kuongeza kiasi cha upatikanaji wa maji jijini Dodoma kwa mipango ya muda mfupi wakati mipango ya muda mrefu ikiendelea.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso alipofungua Mkutano Maalum kati ya Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na viongozi wa mamlaka ya serikali za mitaa kujadili hali ya upatikanaji wa huduma ya maji jijini Dodoma Septemba 05,2024.

Pia Mhe. Aweso amezungumza dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya kumaliza changamoto ya maji jijini Dodoma na zaidi amefafanua kwakina mipango mbalimbali ya serikali ya muda mrefu, muda wa kati na ile ya muda mfupi na jitihada zinazoendelea za kuhakikisha upatikanaji wa maji unaendelea kuboreshwa huku akisisitiza kwamba Dodoma ndio kipaumbele cha sekta ya maji kwa sasa.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn