logo

WAGONJWA WATAKIWA KUWA WADADISI PINDI WANAPOENDA HOSPITALI KUPATA MATIBABU

Wagonjwa wametakiwa kumuuliza daktari anachunguzwa na anatibiwa nini kwa sababu ni haki ya mgonjwa kujua tatizo linalomsumbua wakati anapoanza matibabu.

Akiongea na wagonjwa Siku ya Usalama wa Wagonjwa Duniani leo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof.Abel Makubi, amesema anapaswa kuanza kujimbulisha kwa daktari halafu kueleza historia ya tatizo lake.

"Katika misingi yetu, madaktari tunaanza kumsikiliza mgonjwa, Unapoingia chumba cha daktari, mueleze daktari dalili zote na jinsi unavyojisikia kwa usahihi," amesema Makubi.

Prof.Makubi amebainisha kuwa daktari atauliza maswali yake kwa usahihi kabla ya kukupima na kukuelekeza kufanya vipimo vya maabara au radiolojia.

"Wagonjwa wengi wanakimbilia kwenye vipimo, lakini mgonjwa anapaswa kuanza kumueleza daktari tatizo linalomsumbua," amefafanua Prof Makubi.

Ndugu Salumu Bakari, mkazi wa Dodoma mjini, amepongeza huduma za BMH, akiongeza kuwa.

Bi Mwajuma Ramadhani amesema amekuwa akija kwenye Idara ya Mazoezi ya BMH, akipongeza kuwa hakuna sehemu anayocheleweshwa kwenye mchakato wa huduma BMH.

"Nakuja kila wiki kwa ajili ya mazoezi hakuna sehemu nimepata changamoto katika mchakato wa matibabu," amesema Bi Mwajuma.

Siku ya Usalama wa Mgonjwa Duniani huadhimishwa kila tarehe 17, Septemba. BMH imeadhimisha Siku hii kwa kujielekeza katika kuboresha huduma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn