logo

NMB, TIRA WAANDAA SEMINA YA WAWAKILISHI WA MAKAMPUNI

BENKI Ya NMB Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) leo Mei 11,2023 wameandaa semina kwa wawakilishi wa makampuni yote ya bima nchini iliyowapa uelewa kuhusu Ubora wa mifumo ya upatikanaji wa taarifa kati ya Benki, Kampuni ya Bima na TIRA, Uimara wa kifedha tulionao kama benki, Uwepo wa timu maalum ya wafanyakazi kwaajili ya kushirikiana na kufanya kazi na makampuni ya Bima Na Uwepo wa wabobezi ambao wataiongoza Benki kufanya uwekezaji mzuri na wenye tija kwa makampuni ya Bima.

Semina hiyo imefunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar - Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga mbele ya Kamishna wa Mamlaka ua Usimamizi wa Bima Tanzania - Dkt. Baghayo Saqware , na Naibu kamishna, Bi Khadija Issa Said na tumewakilishwa na Afisa Mkuu wetu Wa Wateja Wakubwa na Serikali - Alfred Shao pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Taasisi- William Makoresho.

@nmbtanzania

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn