logo

RAIS SAMIA AMEFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA MIUNDOMBINU YA ELIMU -WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya kazi kubwa sana katika uwekezaji kwenye Miundombinu ya Elimu.

Waziri Aweso ameyasema hayo baada ya kuzindua mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Kata ya Mwanuzi yenye madarasa nane, jengo la Utawala, Maabara tatu,vyoo kumi, chumba cha kompyuta Maktaba na kichomea taka.

Mradi huu umetumia kiashi cha shilingi 584,280,028.

.

Akizungumza na wazazi na wanafunzi Waziri Aweso amewaasa kusoma kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi wa jamii ya Mtanzania.

Tukio hili limefayika Wilayani Meatu leo tarehe 27 Oktoba 2024 akiendelea na ziara maalumu inayohusisha kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kuzindua Miradi ya Maendeleo ya sekta mbalimbali sambamba na kuzungumza na wananchi kwaniaba ya Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn