logo

WAZIRI BASHE ATAKA VIJANA NA WANAWAKE KUPEWA KIPAUMBELE

WAZIRI wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe Amesema Kama Taifa Tunapaswa kuwapa kipaumbele vijana na wanawake katika harakati za kuchangia uwepo wa Usalama wa Chakula kwa ngazi za Taifa na Bara zima kwa ujumla kwa kutumia uwezo wao wa ubunifu na ufanyaji kazi unaoweza kuchangia maendeleo na uhakika wa upatikanaji wa chakula cha uhakika na salama.

.

Bashe Ameyasema Hayo Leo Mei 12, 2023 Alipokuwa akizindua Rasmi Usajili kwa ajili ya washiriki wa Kongamano la Usalama wa Chakula litakalofanyika Septemba 4-8 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

.

Kabla ya kuzindua usajili huo, Bashe amewaalika wadau wa kilimo wakiwemo Wataalamu wa Masuala ya Mifumo ya Chakula Duniani.

.

Amesema kongamano hilo litaangazia nafasi ya bara la Afrika katika matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha dunia inakuwa na chakula cha uhakika na salama.

.

Waziri Huyo Amesema kuwa Mkutano wa AGRF mwaka huu unafungua milango ya matumizi ya ubunifu katika kuimarisha kilimo pamoja na kufungua milango ya uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu, utungwaji wa sera bora pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa hilo, Bw.Amath Pathe Sene amebainisha kuwa Ubunifu, Sera Bora na Uwekezaji wa Kimkakati ni njia sahihi katika kuhakikisha upatikanaji wa mifumo imara ya chakula.

Sene amesema Septemba 3, wageni wa mkutano huo watapata wasaha wa kutembelea na kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na watanzania na kujionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn