logo

UHALIFU MTANDAONI UMEPUNGUZWA NA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO -ACP MWANGASA

Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania ACP Joshua Mwangasa, amesema kuwa kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kesi nyingi zilizokuwa zikiripotiwa zilikuwa hazifiki mwisho kwa sababu ya kukosekana kwa vifungu vinavyohusisha makosa ya mtandao moja kwa moja kutoka kwenye sheria ya msingi ya Penal Code.

Amesema kuwa utungwaji wa sheria hiyo umekuwa na mafanikio makubwa kwa kupunguza makosa ya uhalifu wa mtandao kwa wananchi kuripoti matukio ya uhalifu wa mtandao katika vituo vya polisi na kushughulikiwa ipasavyo.

ACP Joshua Mwangasa ameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi Tanzania, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wananchi na wadau wengine katika utoaji wa elimu kwa umma na ushughulikiaji wa makosa hayo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn