logo

MBUNGE SALIM ATUMIA VIFAA BINAFSI KUBORESHA BARABARA YA SALI RUAHA

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham tarehe 06 mwezi January,2025 ametoa vifaa na rasilimali zake binafsi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Tarafa ya Ruaha, ambao wamekumbwa na changamoto kubwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kuharibu miundombinu ya barabara muhimu zinazounganisha kata za Ruaha na Sali.

.

Barabara hizo zinazohudumia vijiji sita katika maeneo hayo, uharibifu huo umeleta athari kubwa kwenye usafiri na mawasiliano.

Katika hatua ya haraka ya kusaidia wananchi hao, Mbunge Salim ameanzisha juhudi za kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi, pamoja na matumizi ya gharama zake binafsi, shilingi milioni 60 ili kurahisisha upatikanaji wa usafiri na kuondoa kikwazo cha mawasiliano kilichosababishwa na mvua hizo.

.

"Huu ni mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na ustawi wa wananchi wa Tarafa ya Ruaha, ambapo juhudi hizi zitasaidia kurejesha hali ya kawaida kwa wakazi wa maeneo haya" alisema Mbunge Salim.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mhe.Julius Ningu ameongeza kuwa,

.

“Tunajivunia kuona viongozi wetu wakichukua hatua za haraka na za kipekee ili kusaidia jamii katika nyakati za dharura, msaada huu utaleta mabadiliko makubwa kwa wakazi wa Tarafa ya Ruaha na kuhakikisha wanapata huduma za kimsingi.” alisema.

Kwa sasa, juhudi za ukarabati wa barabara zinaendelea, huku Mhe.Salim akisisitiza kwamba itakuwa ni muhimu kwa wadau wote kushirikiana ili kufanikisha kurejesha hali ya kawaida kwa haraka.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn