BONDIA TYSON FURY ATANGAZA KUSTAAFU KUCHEZA NDONDI
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury jana alitangaza kustaafu ndondi, baada tu ya kupoteza mechi yake ya marudiano dhidi ya bingwa wa WBA Super, WBC na WBO Oleksandr Usyk mwezi Disemba.
Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 36 hapo awali alitangaza kustaafu baada ya kumshinda Dillian Whyte mnamo Aprili mwaka 2022 lakini akarejea miezi sita baadaye.
Fury alifurahia nafasi mbili kama bingwa wa uzani wa juu na ana rekodi ya kushinda mapigano 34, kushindwa mara mbili na sare moja.
Hata hivyo, wadadisi wanaona hatua yake hiyo ni mbinu ya kupata pambano dhidi ya Antony Joshua.
Frank Jordan
12345
123
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

