KILOGRAM 185.35 ZA DAWA ZA KULEVYA ZATEKETEZWA ARUSHA
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, tarehe 15 Januari, 2025, imeteketeza kilogramu 185.35 za dawa za kulevya katika dampo la maji ya chai liliopo wilayani Arumeru, Arusha.
Kati ya dawa zilizoteketezwa, mirungi ilikuwa kilogramu 154.35 na bangi mbichi ilikuwa kilogramu 31 ambazo ziliwahusisha watuhumiwa watano.
Uteketezaji wa dawa hizo umefanyika mara baada ya Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kuelekeza vielelezo hivyo viteketezwe kwani vingeweza kuleta madhara kwa binadamu endapo vingeendelea kuhifadhiwa.
Zoezi la uteketezaji lilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Arusha pamoja na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Arumeru.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

