MTANZANIA DKT.MWAPINGA ACHAGULIWA KATIBU MKUU WA FP-ICGLR NCHINI ANGOLA
Mtanzania Dkt. Deo Mwapinga amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jukwaa la Wabunge wa Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR).
Anachukua jukumu hili kufuatia kuidhinishwa kwa kauli moja na Maspika wa Mabunge wa Nchi nchi wanachama wa ICGLR.
Uidhinishaji wa Dkt. Mwapinga baada ya kuchaguliwa na Maspika wa ICGLR umefanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa FP-ICGLR uliofanyika Luanda Angola leo Aprili 25, 2025 ambapo Wabunge wanaowakilisha mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu walikutana kujadili masuala ya amani, usalama na utawala wa kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa uamuzi wa Maspika kuhusu Uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa FP-ICR.
Katika hotuba yake ya kukubalika nafasi hiyo, Dkt. Mwapinga alitoa shukrani kwa nchi wanachama kwa heshima hiyo, na kuahidi kudumisha Malengo ya FP-ICGLR na kuimarisha ushirikiano wa wabunge katika ukanda wa maziwa Makuu.
"Hii sio tu heshima kwangu bali uthibitisho wa imani kubwa Nchi wananchama wa ICGRL walionayo kwa Tanzania hususani katika kupambania maswala ya ulinzi na amani, ushirikiano wa kikanda na maswala ya demokrasia. Ninakubali jukumu hili kwa ufahamu kamili wa kazi na umuhimu ulio mbele yetu, ambao ni kupigania amani na usalama, kuimarisha diplomasia ya kibunge, kukuza ushirikiano wa kikanda, na kukuza demokrasia, na utawala bora katika eneo letu." alisema Dkt. Deo.
Jukwa la Bunge la ICGLR linajumuisha Mabunge kutoka nchi 12 wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu likiwa na lengo la kusaidia utekelezaji wa itifaki iliyosainiwa mwaka 2006 katika kuimarisha, Ulinzi na Usalama, demokrasia, utawala bora na haki za binadamu.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

