logo

DP WORLD YACHANGIA MAPATO YA TRILION 8.26 BANDARI YA DAR -PROF.MBARAWA

Serikali imetangaza mafanikio ya kushirikisha Sekta Binafsi katika uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kupitia ubia na kampuni za DP World @dpworld na TEAGTL.

.

Mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la mapato ya kodi ya Forodha hadi kufikia shilingi trilioni 8.26 kati ya Julai 2024 hadi Februari 2025, ikilinganishwa na trilioni 7.08 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka 2023/24 kabla ya ubia huo.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa @prof.mbarawa_m akiwasilisha mpango wa mapato na matumizi kwa mwaka 2025/2026 bungeni jijini Dodoma, amesema ushirikiano huo umesaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa bandari kutoka shilingi bilioni 975.01 hadi bilioni 685.16, sawa na punguzo la asilimia 30.

Aidha, muda wa meli kusubiri nangani umepungua kwa kiasi kikubwa kutoka wastani wa siku 46 hadi siku 7 kwa meli za mizigo mchanganyiko, na meli za makasha gatini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku 3, hali inayoimarisha ufanisi wa bandari hiyo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn