DAWA ZA KULEVYA ZAIDI YA KILO 2000 ZIMEKAMATWA KUANZIA JUNI,2024 HADI MEI, 2025 -KAMISHNA JENERALI LYIMO
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema kutokana na uongozi madhubuti wa Serikali ya awamu ya sita, kwa kipindi cha kuanzia Juni, 2024 hadi Mei, 2025, kumekuwa na ongezeko la ukamataji wa dawa za kulevya ukilinganisha na miaka iliyopita.
“Katika kipindi hiki, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, tumekamata dawa za kulevya jumla ya kilogramu 2,301,414.94. Kiasi hiki ni kikubwa ikilingalishwa na kilo 2,050,542.73 zilizokamatwa kati ya Juni, 2023 na Mei, 2024.
.
"Kuanzia Januari hadi Desemba 2024, jumla ya kilo 2,327,983.8 zilikamatwa ikilinganishwa na kilo 1,965,341 zilizokamatwa kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2023.” alisema Lyimo.
.
Kamishna Jenerali ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyohitimishwa na WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

