logo

MAZISHI YA MALKIA ELIZABETH II YAGHARIMU DOLA MILIONI 200

INARIPOTIWA ya Kwamba Mazishi ya Marehemu Malkia Elizabeth II yameigharimu serikali ya Uingereza Kwa Kiasi Cha Takribani Pauni Milioni 162 ( Sawa Na Dola Milioni 200 za Kimarekani), Hii Ni Kwa Mujibu Wa Taarifa ya Kutoka Hazina Iliyotolewa Siku ya Alhamisi Ya Wiki Hii.

.

Mazishi hayo yaliyokuwa Chini ya Serikali ya Uingereza Aliyokuwa akiiongoza Mfalme Huyo yaliyofanyika Septemba 19, yalikuwa ya kwanza nchini Uingereza tangu yale ya Waziri Mkuu wa zamani Winston Churchill mnamo Mwaka 1965.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa Dunia na watu mashuhuri, ilifuatia siku 10 za maombolezo ya kitaifa baada ya malkia kufariki akiwa na umri wa miaka 96 mnamo Septemba 8 baada ya miaka 70 kwenye kiti cha ufalme.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn