logo

MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA ‎HANA UBONGO ATIMIZA UMRI WA MIAKA 20

Msichana Alex Simpson, anayeishi Marekani, alionekana mwenye afya kabisa alipozaliwa Mwezi Novemba 04,2005 walakini, miezi miwili baadaye, madaktari walimgundua na hydranencephaly (hali isiyo ya kawaida na mbaya sana ambayo sehemu za ubongo hazipo au hazijakuzwa)

‎.

‎Madaktari waliiambia familia yake kwamba Alex hangeishi zaidi ya umri wa miaka minne, lakini msichana huyo alikaidi matarajio yote na hivi karibuni amesherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akifikisha miaka 20.

‎.

‎Baba yake, Shawn Simpson, alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha Televisheni nchini humo alisema kuwa, "Alex, ana takribani nusu tu ya ukubwa wa tishu za ubongo za kidole changu na nyingine hazipo kabisa."

‎.

‎Mama yake, Lorena, alieleza maisha ya binti yao kuwa ni “muujiza,” huku akisema,

‎.

‎“Alex alipozaliwa, tuliogopa sana, lakini imani na upendo vilitusaidia kuendelea.”

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn