logo

WAZIRI UMMY AZINDUA JENGO LA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA DODOMA

KATIKA kuadhimisha Siku ya Mchangia Damu Duniani Juni 14, Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu leo Juni 14,2023 amezindua Jengo la Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Kati Dodoma lililopo Itega, Jijini Dodoma.

Hizi ni jitihada endelevu za Serikali kuhakikisha inakuwa na usalama wa damu, upatikanaji wa damu kutoka kwa wachangiaji wa hiari, sehemu salama ya kukusanya, kuhifadhi, kutengeneza mazao ya damu pamoja na kupima magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya damu.

Jengo hilo limejengwa na Serikali kupitia ushirikiano na Serikali ya Korea na ambapo katika uzinduzi wa jengo hilo Balozi wa Korea Nchini Mhe.Kim Sun Pyo ameshiriki.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn