logo

WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA AGRF MWEZI SEPT.2023

RAI imetolewa Kwa Wadau Wa Sekta Ya Mifugo Na Uvuvi Kushiriki Bila Kukosa Katika Mkutano Wa Jukwaa La Mifumo Ya Chakula Afrika (AGRF 2023) unaotarajia Kufanyika Mwezi Septemba 5 Hadi 8 Mwaka Huu.

.

Rai Hiyo imetolewa Na Waziri wa Mifugo Na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega Wakati akizungumza na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Kuelekea Mkutano Huo.

.

Amesema Wadau Wa Mkutano Huo wanapaswa Kuandaa Taarifa za Kampuni Zao Kwa Ufasaha Ili iwe Rahisi kujitangaza na Kuvutia wawekezaji, wafadhili na Kuongeza wigo Wa Biashara Zao Katika Mkutano Huo.

.

Ulega Amesema Fursa Hiyo ya Ushiriki Ni Adhimu hivyo Kila Mdau anapaswa Kuichangamkia Kwa Haraka Na kuitumia Vizuri Kwa kujiandikisha na Kujitokeza Kwa Wingi.

.

"Lengo ni Kupata Wadau wengi Kutoka Tanzania watakaoshiriki Mkutano Huo na Kunufaika na Fursa zake. Ni Vizuri Mkajiandikisha mapema Kwa Kuwa Mara Tuu, Idadi ya Washiriki inayokusudiwa ikitimia dirisha la Usajili Wa AGRF litafungwa" Alisema Ulega.

.

Waziri Huyo Amesema Mkutano Huo unatarajiwa Kuhudhuriwa na Washiriki Zaidi 3,000 Kutoka Sehemu Mbalimbali Duniani Ambao wanajihusisha na Mnyororo Wa Thamani Wa Mifumo ya Chakula.

.

"Lengo la Jukwaa Hilo Ni Kujadili Mikakati na Hatua Madhubuti za Kuimarisha Usalama Wa Chakula barani Africa, Ustawi Wa Uchumi Pamoja Na Uhimilivu na Uendelevu Wa Mifumo ya Chakula barani Africa, Ili kuwezesha Africa Kuzalisha Vyakula Vya Kutosha, kujilisha yenyewe Na Dunia" Alisema Ulega.

.

Aidha, Ulega Amesema Wizara Yake imejipanga Kushiriki kikamilifu Katika Mkutano Huo wa AGRF.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn