logo

MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA VANNILA WAZINDULIWA DODOMA

Kampuni ya Vanilla international Limited imezindua Mradi wa kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma Vanilla village Dodoma katika Kitongoji cha Zamahero Kata ya Mayamaya Wilaya ya Bahi.

Uzinduzi huo umeambatana na utoaji Elimu kwa wananchi wa eneo hilo kuhusu kilimo cha Vanilla ambao umefanyika Julai 22, 2023 katika shamba la kitalu (Green House)kubwa ya kilimo hicho inayotumia njia za kisasa.

Mkurugenzi Mtendaji na muasisi wa makampuni ya Vanilla international Limited ,Simon Mkondya amesema shamba kitalu hilo lipo kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara kuu ya kwenda Arusha lenye ukubwa wa hekta 125.

Mkondya amesema uwekezaji huo unakuja baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia kilimo hicho katika kisiwa cha Zanzibar.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn