logo

INDONESIA: AHUKUMIWA JELA MIAKA 2 KWA KULA NYAMA YA NGURUWE

Mahakama ya Indonesia imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha miaka miwili jela kwa kuchapisha video katika mtandaoni wa TikTok ambayo inaonesha akitamka sala ya Waislamu kabla ya kula nyama ya nguruwe.

Lina Lutfiawati, 33, amekutwa na hatia ya "Kueneza habari zilizokusudiwa kuchochea chuki au uadui wa mtu binafsi/kikundi kwa misingi ya dini"

"Ninajua kuwa nina makosa, lakini sikutarajia adhabu hii," Lutfiawati alisema kupitia MetroTV.

Pia anakabiliwa na faini ya $16,24513,155). Kifungo chake cha jela kinaweza kuongezwa kwa miezi mitatu ikiwa hatalipa.

Indonesia ni taifa kubwa zaidi duniani lenye Waislamu wengi. Na nyama ya nguruwe inachukuliwa kuwa 'haram', au hairuhusiwi, chini ya sheria za Kiislamu.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn