logo

KANISA LAFANYA MISA MAALUM YA KUBARIKI MBWA,PAKA NCHINI MAREKANI

Kanisa moja mjini New York Marekani limefanya misa maalum ya kuwabariki wanyama wa kufugwa majumbani kama vile paka na mbwa.

Waumini wa kanisa hilo waliwapeleka wanyama wao wakiwemo, farasi, mbwa na hata ngamia kupokea baraka ili kusherehekea sikukuu ya mtakatifu Francis wa Assisi, somo mtakatifu wa wanyama na mazingira.

Kanisa hilo limeeleza kuwa, waumini wapatao 1,500 walihudhuria misa hiyo wakiwa na wanyama wao wa kufugwa majumbani.

Je, umewahi kumpeleka mnyama wako kanisani kwa ajili ya kupokea baraka?

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn