POLISI ULANGA WAONYWA, "ACHENI KUWAONEA WAKULIMA"
Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham ameliomba jeshi la Polisi wilayani humo kuacha kuwaonea wananchi jamii ya wakulima pindi wanapopeleka kesi za wafugaji kulisha mifugo katika mashamba yao badala yake wawasaidie kupata haki zao ili kupunguza mvutano kati ya jamii hizo mbili.
Mbunge Salim ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata za Ketaketa na Ilonga alipofika kusikiliza kero zao na wingi wa wananchi walililalanikia jeshi la polisi kuwa halitendi haki katika kesi zao hata kama wakikamata ushahidi na badala yake watuhumiwa wanaachiliwa huru pasipo kuelewa chochote na kupelekea changamoto hiyo ya wafugaji kuendelea kufanya uharibifu huo mara kwa mara na wakulima kupata hasara kila mwaka.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga Imani Mlyapatali amesema ni kweli jeshi hilo limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi hivyo ameagiza wajitathimini kabla ya uongozi wa juu haujaingilia kati kuwachukulia hatu kwani kumnyima haki mwananchi ni uvunjifu wa sheria na inawezakupelekea machafuko katika jamii hizo mbili.
Wilaya ya Ulanga inakabiliwa na changamoto ya wakulima na wafugaji katika vijiji kadhaa kutoka na mifugo kuwa mingi kuliko maeneo rasmi ya malisho ambayo yametengwa hivyo kupelekea wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

