logo

WAZIRI SILAA: MSIWAPANGIE WANANCHI UKUBWA WA VIWANJA WANAVYOVITAKA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa amewataka Wataalamu wa ardhi kutokuwapangia wananchi ukubwa wa viwanja wanavyotaka kununua.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo Wilayani Musoma mkoa wa Mara wakati akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Vijiji 975 nchini.

Waziri Silaa amewataka wataalamu wa ardhi kushirikiana na wananchi ili kuwasaidia katika upimaji shirikishi unaofanywa na makampuni binafsi katika mitaa yao.

Amesema kila mtu awe huru kununua ukubwa wa kiwanja kutokana na uwezo wake na asipangiwe kama makampuni ya upangaji yanavyofanya ili kuepuka uwepo wa viwanja vidogo vidogo katika maeneo yetu.

Aidha, Silaa amewataka wataalamu wa ardhi kutokuwa madalali wa wapima viwanja badala yake kuwapa uelewa na kuwasaidia wananchi kufahamu gharama za upimaji kwa mita za mraba.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn