logo

ABBASI: WATU BILIONI 1.2 WAMEIONA ROYAL TOUR DUNIANI

MWENYEKITI wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, iliyoratibu maandalizi ya filamu ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi, amesema mwaka mmoja leo, tangu filamu hiyo izinduliwe hapa nchini, takribani watu bilioni 1.2 duniani, wameiona au kujihusisha na filamu hiyo kupitia kupata taarifa za vyombo mbalimbali vya habari.

Abbasi ameyasema hayo leo Aprili 28, 2023 alipokutana na wanahabari jijini Dodoma ikiwa ni mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoizindua filamu hiyo jijini Arusha mwaka jana.

“Mwaka mmoja Leo Royal Tour imeleta mafanikio makubwa sana ikiwemo kuongeza watalii nchini maradufu, mapato ya utalii kuongezeka maradufu na hata mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuongeza miruko ya kuja nchini,” alisema Abbasi.

.

Katika Mafanikio yaliyopatikana Kwenye Filamu hiyo,Abbasi Amesema Kwa kipindi cha mwaka mmoja imesababisha kuongezeka kwa watalii nchini ambapo mapato ya jumla ya sekta hii yameongezeka kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na TZS Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani 2,527.77 (sawa la TZS Trilioni 5.82).

.

Aidha, Abbasi Amesema Hamasa ya Royal Tour pia imeongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ambapo amesema kuwa watalii kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 620,867 mwaka 2020 hadi 1,454, 920 Disemba, 2022 sawa na ongezeka la asilimia 57.7 na kufafanua zaidi kuwa kwa takwimu za mpaka Machi, 2023.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn