WATANZANIA TUACHE DHANA POTOFU, TUWAPENDE WENYE 'DOWN SYNDROME' -MKURUGENZI BI.ELLY KITALY
Ikiwa leo ni Machi 21,2024 Siku ya Down Syndrome Duniani, Watanzania wametakiwa kuachana na dhana potofu juu ya watu wenye Down Syndrome hivyo wanapaswa kuwapenda na kuwajali kama ilivyo kwa watu wasio na hali hiyo.
.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya CHADRON'S HOPE FOUNDATION Bi.Elly Kitaly alipokuwa akizungumza na chombo cha habari cha Jordan Media jijini Dodoma.
.
Bi.Elly amesema watu wenye ulemavu hawatakiwi kutengwa kama watu wasiotakiwa katika jamii badala yake, wanatakiwa kujumuishwa katika kila jambo linalowahusu kwani nao wanahitaji kujifunza mambo mbalimbali kama ilivyo kwa watu wengine.
.
""Tumeona katika mataifa mengine,watu wenye Down Syndrome wamefanya vizuri. Mfano nchini Hispania kuna mbunge wa kuchaguliwa ambaye ana hali ya Down Syndrome, tunaamini tukiyajenga Mazingira bora hapa nchini na tukaishi kauli mbiu yetu inayosema "TOKOMEZA DHANA POTOFU ZINAZOPELEKEA UNYANYAPAA" tutatengeneza mazingira ambayo yatawasaidia watu wenye Down Syndrome kufikia hatua wanazostahili" alisema Bi.Elly.
.
Bi.Elly amesema kuwa hapa Tanzania kuna changamoto kubwa sana katika suala la uelewa wa watu wenye Down Syndrome haswa katika dalili za Down Syndrome,ambapo baadhi ya dalili zake ikiwa ni pamoja na kuwa na masikio madogo,pua bapa na kwa watoto,ukuaji wao kuwa tofauti na ule wa watoto wengine.
.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Afya Check Dkt.Isaac Maro amesema ni muhimu sana kwa watoto hao wenye Down Syndrome kushirikishwa kwenye mambo yote yanayofanyika na katika hali na umri walionao, wanastahili kufurahia maisha na kupata elimu kama wengine.
.
""Leo hii tunapoadhimisha Siku ya Down Syndrome tunapeana elimu kuhusiana na haya,lakini tunakumbushana watoto hawa waweze kushirikishwa kwenye mambo yote yanayofanyika na yanayohusu watoto, wazazi tusiwaache nyumbani,tusiwatelekeze,tusiwanyanyapae" alisema Dkt.Isaac.
.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu inaeleza kuwa "TOKOMEZA DHANA POTOFU ZINAZOPELEKEA UNYANYAPAA"
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

