logo

CRDB YASAINI MAKUBALIANO NA CARE INTERNATIONAL

BENKI ya CRDB Jana Mei 05,2023 imesaini makubaliano ya kushirikiana na Shirika la Care International kuwawezesha wanawake kupata mafunzo na mtaji wezeshi kupitia program ya IMBEJU.

Akizungumza kwenye hafla ya makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa ameishukuru Care International kwa utayari wao wa kushirikiana na CRDB Bank Foundation katika program hiyo.

.

Aidha, Tully amewakaribisha wabia wengine kushiriki katika programu hiyo ili kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International, Bi Prudence Masako ameishukuru CRDB Bank Foundation kwa fursa ya kushirikiana kuwawezesha wanawake kupitia programu ya IMBEJU. Prudence alisema amesema ushirikiano huo utakwenda kusaidia juhudi zao za kukabiliana na umasikini.

Program ya IMBEJU ilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Machi 12 mwaka huu na kufungua dirisha la maombi ambapo kwa upande wa biashara bunifu za vijana maombi 706 yamepokelewa na 196 kukidhi vigezo vya kuendelea na hatua ya pili.

Tully amesema dirisha la maombi kwa upande wa wanawake wafanyabiashara bado lipo wazi na kuwataka wanawake kuendelea kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia program ya IMBEJU.

@crdbbankplc

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn